Tufanye mazoezi kuimarisha afya zetu-Rais Dkt.Mwinyi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema kuwa,tafiti zimeonesha kuwa mazoezi yanasaidia kwa kiasi kikubwa kujenga Afya ya Mwili ,afya ya akili na kuondosha Msongo wa Mawazo na kusisitiza jamii kuwa na utaratibu wa kufanya mazoezi kila siku.
Rais Dkt.Mwinyi ameyasema hayo alipozungumza baada ya Kuongoza matembezi ya Afya yalioandaliwa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Taasisi ya Pharm Access ikiwa ni kampeni maalum ya kudhibiti Maradhi yasioambukiza kwa jamii yalioanzia Kiembe Samaki kwa Boutros hadi Uwanja Mao Tse Tung Wilaya ya Mjini.

Aidha, Rais Dk.Mwinyi amesema Serikali itaendelea kuchukua juhudi maalum kuhakikisha inapunguza kasi ya ongezeko la Maradhi yasiombukiza hapa nchini.

Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa Takwimu za Wizara ya Afya zimeeleza kuwa kuna Ongezeko la Maradhi Yasioambukiza kwa kiwango kikubwa ikwemo Kisukari, Presha , Uzito na Unene uliopitiliza na shinikizo la damu kunakosababishwa na watu wengi kutofanya mazoezi .

Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa kutofanya Mazoezi kwa Wananchi walio wengi kunarejesha nyuma juhudi za Serikali za kudhibiti Maradhi hayo na kupunguza kasi ya kuleta Maendeleo.

Rais Dkt.Mwinyi ametoa wito kwa kila mmoja kuchukua hatua ya kupunguza matumizi ya vyakula vya wanga na mafuta kukabiliana na maradhi hayo.

Vilevile Rais Dkt. Mwinyi ameshauri kuendelezwa na kupangiwa Utaratibu mzuri wa Matembezi ya pamoja na mazoezi .

Kwa upande mwingine Waziri wa Afya, Nassor Ahmed Mazroui amesema Dhamira ya Serikali ni kuona wananchi wote wana afya njema na kutambua kuwa suala la kufanya mazoezi sio anasa na Wizara inajiandaa kuwa na siku maalum ya mazoezi kila mwezi.
Ametoa rai kwa taasisi za umma na binafsi kuandaa utaratibu wa kuwa na siku maalum ya kufanya mazoezi.

Matembezi hayo ya afya yamebeba kaulimbiu inayosema "Chagua Mazoezi kuwa Sehemu ya Maisha ".

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news