Tukutane kujadili Kesho ya Nchi yetu,vijana ndiyo nguzo ya nchi-Waziri Ridhiwani Kikwete
DAR-Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi,Vijana, Ajira na wenye Ulemavu), Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Kongamano la Vijana ambalo litaangazia uhakiki wa rasimu ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Kongamano hilo linatarajiwa kufanyika Desemba 18,2024 saa 2:00 asubuhi katika Makumbusho ya Taifa iliyopo Posta jijini Dar es Salaam.