DAR-Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tanzania Bara, Tundu Lissu hii leo Desemba 17, 2024 amefika katika Ofisi za Makao Makuu ya chama hicho zilizopo Mikocheni mkoani Dar es Salaam kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa chama hicho Taifa katika uchaguzi wa ndani unaotarajiwa kufanyika Januari 21, 2025.
Aidha,mara baada ya kuchukua fomu, Tundu Lissu amesema kuwa, uchaguzi huo utatengeneza ukurasa mpya katika chama hicho huku akiahidi kuwa katika uongozi wake atahakikisha anaongoza mapambano ya kupigania haki.
Vilevile kupiga vita vitendo vya uvunjifu wa amani pamoja na kuhakikisha viongozi wanaotenda haki ndio wanaoshika vyazifa za uongozi.
Lissu amechukua fomu ikiwa ni siku moja baada ya Katibu Mkuu wa chama hicho, John Mnyika kuwatangazia wanachama wa chama hicho kuhusu mchakato wa uchaguzi wa viongozi mbalimbali wa chama.
Sambamba na mabaraza kwa ngazi ya Taifa pamoja na utaratibu wa kupata fomu za kugombea katika uchaguzi huo ambao unatarajiwa kufanyika hivi karibuni.