ZANZIBAR-Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi amezisisitiza jumuiya za chama hicho kuzitumia rasilimali vizuri kwa lengo la kukijengea uwezo kiuchumi.


Dkt.Mwinyi ameupongeza Uongozi wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Kichama Mfenesini kwa Kujenga Jengo la kisasa la jumuiya hiyo na kuwa na dhamira ya kuanzisha miradi ya ushonaji na ukumbi wa shughuli mbalimbali.
Halikadhalika Dkt.Mwinyi ameahidi kwa Chama Cha Mapinduzi kuunga mkono miradi ya kimkakati ya itakayoanzishwa na jumuiya zote za chama hicho ili ziweze kujitegemea.