DAR-Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya TEHAMA Tanzania (ICTC), Dkt. Nkundwe Mwasaga amesema kuwa, Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi nchini (PDPC) ipo kuhakikisha watu wanashiriki kikamilifu katika uchumi wa kidigitali.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya TEHAMA, Dkt.Nkundwe Mwasaga.
Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi nchini ilianzishwa rasmi Mei 1, 2023 kufuatia kupitishwa kwa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi Na. 11, 2022.
Aidha,tume ilianza utekelezaji wa majukumu yake kama matokeo ya utekelezaji wa Sheria hiyo na kuanzishwa rasmi majukumu yake.
"PDPC wapo kuhakikisha wanajenga mazingira ambayo watu wataweza kujisikia vizuri kushiriki katika Uchumi wa Dijitali,” amesisitiza Dkt.Mwasaga, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya TEHAMA; Tazama video chini