DODOMA-Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu -Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,Mhe. Ridhiwani Kikwete ameshiriki mashindano ya Usomaji wa Quraan Takatifu kwa Wenye Ulemavu yaliyoandaliwa na Taasisi ya Riziki Lulida jijini Dodoma.
Katika mashindano hayo ambayo yalikutanisha Wenye Ulemavu kutoka makundi mbalimbali,Mheshimiwa Waziri Ridhiwani Kikwete alitoa salamu za Serikali na kuwakumbusha kazi nzuri anayoifanya Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri Ya Muungano ya Tanzania.
Miongoni mwa kazi hizo ni pamoja na Mkakati wa kusimamia Haki na Ustawi wa Wenye Ualbino, Sera ya Usimamizi wa Teknolojia saidizi na mapitio ya sera mbalimbali zinazosimamia maslahi ya Wenye Ulemavu ikiwemo sera ambazo haziendani na mazingira ya sasa.
Waziri Ridhiwani Kikwete kwa upande wa wizara alieleza walipofikia katika kila maelekezo ya Mheshimiwa Rais, Ilani ya Uchaguzi na miongozo mingi imetolewa.
Pia,aliendelea kumpongeza mwaandaaji, Bi. Riziki Lulida, na taasisi yake na Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA) na washiriki na kwa upekee Mheshimiwa Rais kwa kuunga mkono jambo hilo kwa kuchangia shilingi milioni 15 kwa vijana washiriki 30, walioshiriki usomaji wa kitabu hicho kitakatifu.
Tags
Habari
Mashindano ya Usomaji wa Quraan Takatifu
Quraan Takatifu
Ridhiwani Kikwete
Watu wenye Ulemavu