DODOMA-Baadhi ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamepata ajali na kukimbizwa Hospitali kwa matibabu.
Ajali hiyo imetokea leo asubuhi Desemba 6,2024 wakati moja ya basi lililokuwa limebeba wabunge wanaoelekea kwenye mashindano ya michezo ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki mjini Mombasa nchini Kenya limepata ajali.
Ni kwa kugongana na lori la mzigo maeneo ya Mbande huko Kongwa jijini Dodoma.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Bunge imesema,majeruhi wa ajali hiyo ambao ni maafisa wa Bunge wamekimbizwa Hospitali ya Uhuru na Hospitali ya Benjamin Mkapa za mkoani Dodoma.
Inakadiriwa kuwa wabunge waliopata ajali walikuwa 50 katika basi hilo ambalo nj kati ya manne yanayowasafirisha kutoka Kampuni ya Shabiby.