ZANZIBAR-Kocha wa Zanzibar Heroes, Hemed Suleiman (Morocco) ambaye pia ni kocha wa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) ametangaza kikosi cha wachezaji 30 cha Zanzibar Heroes kwa ajili ya michuano ya Mapinduzi Cup 2025, ambayo rasmi itaanza Januari 3 hadi Januari 13, 2025 kisiwani Pemba.
Morocco ambaye ataiongoza Zanzibar Heroes anakuwa kocha wa kwanza kutangaza kikosi chake kwa Michuano hiyo kwa mwaka 2025 ambayo itashirikisha timu za taifa za Tanzania Bara, Burkina Fasso, Burundi, Kenya, Uganda na wenyeji Zanzibar.
Kikosi hicho hakijajumuisha wachezaji wa Simba SC na Yanga SC ambazo zitakuwa na majukumu ya michuano ya CAF wakati wa mashindano hayo ingawa Sheikhan Khamis ndio mchezaji pekee kutoka Yanga kuitwa.
MAGOLIKIPA
1. Ahmed Ali Suleiman 'Salula' (Uhamiaji FC)
2. Suleiman Said Abraham (KVZ FC)
3. Yakubu Suleiman Ali (JKT Tanzania)
MABEKI
4. Salum Khamis Salum. 'Gado' (JKT Tanzania)
5. Abdallah Said Ali 'Laso'. (KMC FC)
6. Suwed Juma Hussein 'Aguero' (JKU SC)
7. Adeyem Saleh Ahmed 'Machupa (Geita Gold FC)
8. Abdulhalim Abdalla Juma (Chipukizi United)
9. Abdulrahim Seif Bausi (JKT Tanzania)
10. Ibrahim Ame 'Varane' (Mashujaa FC)
11. Abdallah Kheir 'Sebo' (Azam FC)
12. Mukrim Issa Abdallah 'Miranda' (Coastal Union)
13. Abdulmalik Adam Zakaria 'Agreiy' (Mashujaa FC)
14. Baraka Mtui 'Popa' (Mashujaa FC)
15. Laurian Omar Makame (Fountain Gate FC)
VIUNGO
16. Khalid Habib Iddi (Singida BS)
17. Abdulziz Makame 'Bui' (Geita Gold FC)
18. Abdallah Yassin 'Kulandana' (Fountain Gate FC)
19. Hassan Nassor Maulid (JKT Tanzania)
20. Suleiman Saleh Abdalla (KVZ FC)
21. Feisal Salum Abdallah 'Feitoto' (Azam FC)
22. Hassan Haji Ali 'Cheda' (Mashujaa FC)
23. Abdallah Idd Mtumwa 'Pina' (Mlandege FC)
24. Saleh Massoud Abdallah "Tumbo' (Pamba Jiji FC)
25. Sheikhan Ibrahim Khamis (Yanga SC)
26. Ali Khatib "Inzaghi (Uhamiaji FC)
WASHAMBULIAJI
27. Ibrahim Hamad Hilika (Tabora United)
28. Maabad Maulid Maabad (Coastal Union)
29. Ibrahim Abdallah Ali 'Mkoko' (Namungo FC)
30. Rashid Said Salum (Zimamoto FC).