DODOMA-Wakili Mkuu wa Serikali Dkt. Ally Possi ameshiriki kikao kazi cha Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Wakurugenzi wa Divisheni/Idara na Wakuu wa Vitengo vya huduma za Sheria Serikalini.
Katika kikao hicho Wakili Mkuu wa Serikali aliwasilisha mada kuhusu namna ya Uendeshaji wa Mashauri ya Serikali.
Kikao kati ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Wakurugenzi wa Divisheni/Idara na Wakuu wa Vitengo vya huduma za Sheria Serikalini kilifanyika tarehe 06 Desemba, 2024 Jijini Dodoma.