Wakulima Kiteto wahamasika matumizi ya mbolea na mbegu za ruzuku msimu huu wa kilimo

MANYARA-Wakulima 137 wilayani Kiteto wamehamasika kutumia mbolea na mbegu za ruzuku kwa msimu wa kilimo 2024/2025.
Hayo yamebainishwa na Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) Kanda ya Kaskazini, Gothard Liampawe alipokuwa akitoa taarifa ya ushiriki wa Mamlaka katika kongamano la uzinduzi wa msimu wa kilimo wa mwaka 2024/25 lililofanyika tarehe 20 Desemba 2024, wilayani Kiteto, mkoa wa Manyara.

Kongamano hilo liliendeshwa chini ya uongozi wa Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya, akiwa mgeni rasmi.
Katika kongamano hilo, Meneja wa TFRA Kanda Liampawe aliwahamasisha wakulima kuchangamkia fursa ya kupata mbolea na mbegu kwa bei ya ruzuku inayotolewa na serikali kupitia mfumo rasmi wa kidigitali.

Amesema kupitia kongamano hilo, wakulima wapya 75 walijisajili katika mfumo wa ruzuku ili waweze kunufaika na mbolea na mbegu bora zinazotolewa kwa bei ya ruzuku.

Aliongeza kuwa, wakulima 10 walihuisha taarifa zao ndani ya mfumo huo kutokana na kuingeza maeneo ya kulima ili kuendelea kufaidika na mpango huo wa serikali.

Bwana Liampawe alisisitiza umuhimu wa ushirikiano baina ya viongozi wa Wilaya na Mamlaka za Serikali katika kuhamasisha wakulima kujisajili kwenye mfumo wa ruzuku.

"Hakuna njia mbadala ya kunufaika na ruzuku ya mbolea na mbegu bila kujisajili kupitia mfumo rasmi. Hii ni nafasi ya kipekee kwa wakulima kuongeza tija na uzalishaji katika kilimo."
Kongamano hilo lilikuwa fursa muhimu kwa wakulima wa Kiteto kufahamu manufaa ya ruzuku ya mbolea na mbegu, huku likisisitiza umuhimu wa wadau wote kushirikiana ili kuhakikisha kilimo kinaleta tija na ustawi kwa wakulima nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news