Wanawake Chalinze wamshukuru Rais Dkt.Samia kwa nishati safi ya kupikia

PWANI-Wanawake katika Jimbo la Chalinze lililopo Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze mkoani Pwani wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa nishati safi ya kupikia.

Shukrani hizo zimetolwa na Bi. Lilian Skawa kwa niaba ya wanawake wa Chalinze mbele ya Mbunge wa Jimbo la Chalinze na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu ,Kazi Ajira na Wenye Ulemavu,Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete wakati wakipokea majiko ya gesi 118 kwa mama lishe wa kata 15 za Jimbo la Chalinze.
Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete amesema, lengo kubwa la kugawa majiko hayo ya gesi ni kuunga mkono juhudi za Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kutunza mazingira na kuwafanya wananchi kuondokana na matumizi ya nishati chafu.
"Sasa mtakwenda kupika chakula kwa haraka na kwa usafi na hii itasaidia katika shughuli zenu kwa pamoja tutamuunga Mhe. Rais kwenye uhamasishaji wa matumizi ya nishati safi ya kupikia, ambayo italinda afya zenu pia," amesema.Afisa Maendeleo ya Jamii na mratibu wa dawati la Jinsia wa Halmashauri hiyo,Recho Mnguruta amesemammajiko hayo yatakwenda kuwasaidia Wanawake wajasiriamali hao kuondokana na kutumia kuni na mkaa.

Naye Bi. Lilian Skawa mkazi wa Msata amemshukuru Mbunge huyo wa Jimbo hilo kwa kuwapatia majiko hayo ambayo yatawarahisishia kwenye kazi yao kupika kwa haraka na kuwapatia wateja wao chakula cha moto muda wote.
Amesema, kipindi cha mvua walikuwa wanakabiliana na changamoto ya mkaa ambao wanapata kwa shida na ukiwa umelowa hivyo kwasasa wanakwenda kuwa na mabadiliko ya kupika kwa wakati chakula na kwa hali ya usafi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news