Watendaji wa halmashauri wapigwa msasa matokeo ya Sensa ya mwaka 2022

JOSEPHINE MAJURA
NA CHEDAIWE MSUYA

NAIBU Waziri wa Fedha Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), amesema kuwa matokeo ya Sensa ya Mwaka 2022 yanalenga kuisaidia Serikali na wadau wengine kufuatilia na kufanya tathmini juu ya utekelezaji wa mipango na programu za maendeleo katika Sekta zote nchini.
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Mwanaidi Ali Khamis (Mb), akiagana na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya Vijijini, Mhe. Oran Njeza, baada ya kumaliza kufungua mafunzo ya Usambazaji na Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 kwa Viongozi na Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya vijijini, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Mbalizi Mbeya.

Hayo yameelezwa kwa niaba yake na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis (Mb), wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Usambazaji na Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022, yaliyotolewa kwa Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya Vijijini yaliyofanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Mbalizi mkoani Mbeya.
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Mwanaidi Ali Khamis (Mb), akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Usambazaji na Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 kwa Viongozi na Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya vijijini, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Mbalizi Mbeya.

“Matokeo hayo ndio yatakuwa dira yetu katika kufanya maamuzi yote ya msingi yanayohusu uanzishaji wa miradi mipya, uimarishaji na kuboresha utoaji wa huduma mbalimbali kwa wananchi zikiwemo za kijamii kama elimu, afya, maji na huduma nyingine kama za kiuchumi na miundombinu,” alisema Mhe. Mwanaidi.
Baadhi ya Viongozi na Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya Vijijini, wakifuatilia wasilisho lililotolewa wakati wa mafunzo ya Usambazaji na Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 kwa Viongozi na Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya vijijini, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Mbalizi Mbeya.

Aidha, aliwasisitiza washiriki wa mafunzo hayo watendaji na viongozi mbalimbali kutumia matokeo ya sensa na takwimu mbalimbali wanapozungumza na wananchi ili kuwajengea uelewa wa umuhimu wa takwimu katika maendeleo.
Naibu Waziri Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Mwanaidi Ali Khamis (Mb), akiteta jambo na Mkurugenzi wa Mifumo ya Taarifa za Kijiografia kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw. Benedict Mugumbi, wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Usambazaji na Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 kwa viongozi na watendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mbeya vijijini, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Mbalizi Mbeya.

Mhe. Naibu Waziri Mwanaidi, aliwataka pia washiriki wa mafunzo hayo kufikisha elimu kwa wananchi kupitia vikao vinavyowakutanisha viongozi, wataalamu na wananchi na wadau wa maendeleo ili kujenga uelewa wa kuyafahamu masuala hayo.
Mkurugenzi wa Mifumo ya Taarifa za Kijiografia kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw. Benedict Mugumbi, akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Usambazaji na Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 kwa Viongozi na Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya vijijini, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Mbalizi Mbeya.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mifumo ya Taarifa za Kijiografia kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw. Benedict Mugumbi kwa niaba ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali, alisema kuwa ofisi hiyo ipo tayari kutoa mafunzo hayo katika mikoa mbalimbali ili kuhakikisha mafunzo hayo yanafika kwa wananchi wote.

Mafunzo ya usambazaji na matumizi ya matokeo ya sensa ya watu na makazi yamefanyika kwa ushirikiano kati ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Mbeya Vijijini.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti ambaye ni Mbunge wa Mbeya Vijijini, Mhe. Oran Njeza akizungumza wakati wa mafunzo ya Usambazaji na Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 kwa Viongozi na Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya vijijini, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Mbalizi Mbeya.

Akizungumza katika tukio hilo, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti ambaye ni Mbunge wa Mbeya Vijijini Mhe. Oran Njeza aliishukuru Serikali kwa kuendelea kupeleka fedha ambazo zinasaidia kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo jimboni humo.
Naibu Waziri Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Mwanaidi Ali Khamis (Mb) (katikati), Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya Vijijini Mhe. Oran Njeza (kushoto), Mkurugenzi wa Mifumo ya Taarifa za Kijiografia kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw. Benedict Mugumbi (kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi na Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya Vijijini, baada ya kumalizika kwa mafunzo ya Usambazaji na Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022, kilichofanyika katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Mbalizi Mbeya.

Aidha, aliiomba Serikali kuendelea kutenga fedha kwa ajili ya kulipa fidia mbalimbali kwa wananchi jimboni humo ambao walipisha maeneo yao kwa Serikali ili yaweze kutumiwa na Serikali kwa ajili ya kuyaendeleza kupitia miradi mbalimbali ikiwemo upanuaji wa barabara.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news