DAR-Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe Hamis Mwinjuma amewataka Wakandarasi wa viwanja vya mazoezi ya CHAN 2025 kuhakikisha wanaongeza nguvu kazi ili kazi iliyobakia imalizike kwa wakati.
Mhe. Mwinjuma ameyasema hayo Desemba 24, 2024 ikiwa ni kwenye mwendelezo wa ziara yake ya ukaguzi wa maboresho ya viwanja vya mazoezi kwa ajili ya mashindano ya CHAN 2025.
Katika ziara hiyo, Mhe Mwinjuna ametembelea Uwanja wa Mej Jenerali Isamuyo na Kiwanja cha Law School.
Aidha, Mhe Mwinjuna amesema ameridhishwa na jitihada zote zinazofanywa na mkandarasi na ana imani kuwa vitu vyote vinavyotakiwa kwa vigezo vya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika vitafikiwa na viwanja hivyo vitakabidhiwa tarehe 21 Januari, 2025.