Waziri Aweso anadi miradi ya maji Korea

SEOUL-Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa H. Aweso (Mb) ametembelea na kufanya mazungumzo na Benki ya EXIM ya Korea ambayo imefadhili utekelezaji wa miradi ya Majitaka nchini Tanzania yenye jumla ya Dola za Kimarekani Milioni 248.3 (Mkoa wa Dar es Salaam 90 $US milioni, Dodoma 70 $US million; na Iringa 88.3 $US million).
Katika mazungumzo hayo, Makamu wa Rais wa Benki hiyo amesema kupitia EDCF na Mifuko mingine Serikali ya Korea itaendelea kuisapoti Serikali ya Tanzania kupitia Sekta ya Maji katika uwekezaji zaidi wa utekelezaji wa Miradi ya Maji.

Utelezaji wa miradi hiyo utaimarisha huduma za Usafi wa Mazingira, kuondoa na kutibu majitaka.

Vilevile, Tanzania imepata msaada wa Dola za Kimarekani milioni 8 ambazo zitajenga mfumo wa kusimamia huduma za maji yaani Smart Water Management System (SWMS) katika Mamlaka ya Maji Iringa kutoka Korea Environmental Industry and Technology Institute (KEITI).
Pia, Kupitia mfumo huo, IRUWASA itakuwa Mamlaka ya Maji ya kwanza Nchi kutumia mfumo huo ambao utaongeza ufanisi katika kudhibiti upotevu wa maji, kuimarisha ukusanyaji wa mapato na kuimarisha huduma ya maji.

Kupitia ziara hiyo, Waziri Aweso ameimarisha ushirikiano na wadau wa maji Nchini Korea ambao ni K-Water na makampuni mbalimbali hali ambayo imefungua fursa zaidi za kushirikiana katika kujengea uwezo watumishi na Taasisi za Maji ikiwa ni pamoja na kuandaa miradi na kutafuta fedha za utekelezaji

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news