Waziri Chana awataka watumishi kuwa wabunifu

NA HAPPINESS SHAYO

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) amewaasa watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Taasisi zake kutekeleza majukumu yao kwa ubunifu katika kuendeleza Sekta ya Maliasili na Utalii.
Ameyasema hayo leo Desemba 21,2024 katika Mkutano wa 32 wa Baraza la Wafanyakazi uliofanyika ukumbi wa Mikutano wa Kituo cha Utalii Ngorongoro jijini Arusha.

"Lazima tufanye kazi za Watanzania ambao wametupa dhamana kwa ari na ubunifu wa hali ya juu," Mhe. Chana amesisitiza.
Aidha, ameitaka menejimenti ya Wizara ya Maliasili na Utalii kuhakikisha inaendelea kusikiliza madai na changamoto za Utumishi na kuzitatua.

Amewataka kutumia fursa ya baraza hilo kujadili hoja za kiutumishi, mustakabali ya hali za Utumishi na utekelezaji wa malengo ya Sekta ya Maliasili na Utalii.
Katika hatua nyingine,Mhe. Chana ameielekeza menejimenti na Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii kuweka mazingira wezeshi kuvutia wawekezaji,Kusimamia na kulinda malikale kwa manufaa ya Taifa na kuimarisha usimamizi na ulinzi wa rasilimali kwa faida ya kizazi cha sasa na baadaye.
Naye, Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii,Dkt. Hassan Abbasi amesema Wizara imeendelea kuweka kipaumbele changamoto na maslahi ya watumishi sambamba na kuweka mazingira wezeshi ya utendaji kazi.
"Tunahakikisha kila panapowezekana tunakwenda vizuri, Serikali yetu inaendelea kutuwezesha kwa hiyo kazi inapaswa kuendelea," amesema Dkt. Abbasi.
Kikao hicho kimehudhuriwa na Menejimenti ya Wizara ya Maliasili na Utalii, Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara ya Maliasili na Utalii, Viongozi wa wa TUGHE Taifa na Mkoa pamoja na watendaji kutoka Taasisi za Wizara ya Maliasili na Utalii.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news