Waziri Dkt.Nchemba afanya mazungumzo na Ujumbe kutoka Benki ya Dunia

DAR-Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), ameongoza ujumbe wa Tanzania katika kikao kati ya Serikali na Ujumbe wa Wataalam kutoka Benki ya Dunia, ukiongozwa na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bw. Nathan Belete, kilichojadili vipaumbele vya miradi ya nchi itakayotekelezwa kupitia Dirisha Jipya la IDA21, kikao kilichofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha jijini Dar es Salaam. 
Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Kamishna wa Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, Bw. Rished Bade na Viongozi wengine waandamizi wa Serikali kutoka Wizara ya Fedha na Benki ya Dunia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news