Waziri Dkt.Nchemba ahitimisha ziara nchini Oman

MUSCAT-Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amehitimisha ziara yake ya siku mbili nchini Oman ambapo akiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Muscat – Oman, akielekea nchini Saudi Arabia ambako atakuwa na ziara nyingine ya kikazi, aliagwa na Mhe. Balozi wa Tanzania nchini humo, Mhe. Fatma Rajab.
Akiwa nchini Oman, pamoja na mambo mengine, Mhe. Dkt. Nchemba alitia saini Mkataba wa Kuondoa Utozaji Kodi ya Mapato Mara Mbili na Kuzuia Ukwepaji Kodi, ujulikanao kama An Agreement for the Elimination of Double Taxation with Respect to Taxes on Income and Prevention of Tax Avoidance and Evasion, wenye lengo la kukuza biashara na uwekezaji kati ya nchi hizo mbili.

Aidha, Mhe. Dkt. Nchemba, amewasili nchini Saudi Arabia kwa ajili ya kushiriki katika Jukwaa la Biashara na Uwekezaji, linalotarajiwa kufanyika katika Makao Makuu ya Chemba ya Biashara Riyadh, Saudi Arabia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news