DODOMA-Waziri wa Katiba na Sheria,Mhe. Palamagamba Kabudi amefungua kikao kazi cha Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Hamza S. Johari na Wakurugenzi wa Divisheni/Idara na Wakuu wa Vitengo vya Sheria Serikalini.
Kikao kazi hicho kimefanyika leo Desemba 6,2024 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Jiji Dodoma, uliopo Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.
Akizungumza katika ufunguzi wa kikao hicho Mhe. Kabudi amewataka Mawakili wa Serikali kufanya kazi kwa mshikamano na kutambua kuwa wao ni wawakilishi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika maeneo yao ya kazi.
Tags
Habari
Mwanasheria Mkuu wa Serikali
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali
Wizara ya Katiba na Sheria