Waziri Kombo aongoza Mkutano wa Dharura wa Kamati ya Mawaziri wa SADC TROIKA

DAR-Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.) ameongoza ujumbe wa Tanzania kushiriki Mkutano wa Dharura wa Kamati ya Mawaziri wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika uliofanyika kwa njia ya mtandao la Mawaziri tarehe 9 Desemba 2024, kwa njia ya mtandao.
Mkutano huo ambao umewakutanisha Mawaziri wa Mambo ya Nje na Ulinzi wa Nchi Wanachama za Tanzania ambayo ni Mwenyekiti wa Asasi hiyo, Malawi ambayo ni Mwenyekiti ajaye na Zambia ambayo ni Mwenyekiti anayemaliza muda wake umejikita katika kujadili hali ya ulinzi na usalama Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) hususani bajeti ya Misheni ya kanda iliyopo nchini humo kwa kipindi cha kuanzia mwezi Desemba 2024 hadi Desemba 2025.
Wakati wa Mkutano huo Waziri Kombo amesisitiza umuhimu wa Nchi Wanachama kuendelea kuchangia Misheni hiyo kwa Wizara za Fedha kutoa kipaumbele kwa michango hiyo pamoja na kuonanisha juhudi za kijeshi na kidiplomasia.

Taarifa ya Kikao hicho itawasilishwa katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC kitakachofanyika tarehe 11 Desemba, 2024 na kuongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Tanzania na Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC.
Kikao hicho kilichotanguliwa na Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama kilichoongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara, ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mwenyekiti wa Kamati ya Makatibu Wakuu wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama Balozi, Dkt. Samwel Shelukindo kilichotangulia kikao cha Mawaziri.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news