Waziri Kombo asaini kitabu cha maombolezo Ubalozi wa India

DAR-Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.) amesaini Kitabu cha Maombolezo Ubalozi wa India nchini kufuatia kifo cha Waziri Mkuu mstaafu wa India, Mhe. Manmohan Singh kilichotokea Desemba 26, 2024.
Waziri Kombo aliwasili ubalozini hapo Desemba, 31, 2024 na kupokewa na Balozi wa India nchini, Mhe. Bishwadip Dey.
Balozi Kombo aliwasilisha salamu za pole kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo alimweleza Hayati Manmohan kama kiongozi mahiri aliyeimarisha uhusiano mzuri na Tanzania katika mihula miwili ya utawala wake kuanzia mwaka 2004 hadi 2014.
Katika kipindi hicho cha ungozi wake Hayati Manmohan aliwahi kufanya ziara nchini Tanzania wakati wa Serikali ya awamu ya nne iliyokuwa ikiongozwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news