ABU DHABI-Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo ameshiriki hafla ya Maadhimisho ya Siku ya Taifa la UAE iliyoandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya UAE akiwa ni Mgeni wa Heshima.

Washiriki wengine walikuwa ni wanadiplomasia walioko nchini UAE na viongozi wengine wa Serikali ya UAE.
Katika hafla hiyo Balozi Kombo alikutana na kusalimiana na Mheshimiwa Sheikh Abdullah Al Nahyan, Mhe Makhboot na Mhe Reem Al Hashimy pamoja na viongozi wengine wa Serikali ya UAE.

Tarehe 02 Desemba, 2024 UAE iliadhimisha miaka 53 ya Umoja wao tangu ulipoasisiwa mwaka 1971.