Waziri Mkuu akagua maendeleo ya mradi wa maji Kisesa mkoani Mwanza

MWANZA-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Desemba 21, 2024 amewasili mkoani Mwanza kwa ziara ya kikazi na kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa tenki la kuhifadhi maji la Kisesa, mkoani Mwanza ikiwa ni Mpango wa muda wa kati wa kuboresha huduma ya maji Mwanza ambao unatarajiwa kugharimu shilingi bilioni 3.54.
Mradi huo ambao unafadhiliwa na Serikali ya Tanzania na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (France Development Agency) hadi kukamilika kwake na mpaka sasa umefikia asilimia 93 na unatarajiwa kuhudumia wananchi 75,000 wa maeneo ya Kisesa Bujora, Igudija na swhemu za jirani.
Akizungumza na wananchi wa eneo la Kisesa baada ya kukagua mradi huo Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanya kazi kubwa ya utekelezaji wa miradi mikubwa inayowagusa wananchi moja kwa moja kwenye sekta za elimu, afya, maji, kilimo, uvuvi na barabara.
Kwa upande wake, Waziri wa Maji Jumaa Aweso amesema wizara hiyo itaendelea kusimamia maagizo ya Rais Dkt. Samia ya kuhakikisha wananchi wanapata maji katika maeneo yao.“Mheshimiwa Rais Dkt. Samia alisema hataki kuona wananchi wanateseka kutafuta maji”.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) Nelly Msuya amesema kuwa Matenki mengine yatajengwa katika maeneo ya vilima vinavyozunguka Mji wa Mwanza ikiwemo Nyamazobe (lita milioni 10), Buhongwa (Lita milioni 5), Fumagila (Lita milioni 10) na Usagara (lita milioni 1). “Utekelezaji wa mradi huu wa thamani ya Tsh. Bilioni 49 umeanza na unatarajiwa kukamilika ndani ya miaka miwili (2) ifikapo Desemba 2026”.
Aidha, amesema kuwa ujenzi wa tenki la Kisesa lenye ujazo wa lita milioni 5, unatarajiwa kukamilika ifikapo Februari, 2025.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news