KIGOMA-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Desemba 5, 2024 amemwakilisha Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango kwenye Mahafali ya 43 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania yanayofanyika katika viwanja vya Kawawa mkoani Kigoma.
Mahafali hayo pia yanahitimisha maadhimisho ya miaka 30 tangu chuo hicho kianze kutoa mafunzo mwaka 1994.