Waziri Mkuu amwakilisha Rais Dkt.Samia mkutano wa 21 wa Chama cha Majaji na Mahakimu wa Afrika Mashariki
ARUSHA-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Disemba 03, 2024 amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa Ishirini na Moja wa Chama cha Majaji na Mahakimu wa Afrika Mashariki.
Mkutano huo unafanyika katika ukumbi wa mikutano wa Hotel ya Grand Melia, jijini Arusha.