DAR-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Desemba 02, 2024 ameshiriki katika tukio la kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kigamboni na Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani Kanda ya Afrika, Dkt. Faustine Ndugulile.
Tukio hilo ambalo limefanyika katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam limeongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.