Waziri Mkuu azindua nyumba 109 za waathirika wa maafa ya maporomoko ya tope Hanang'

MANYARA-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Desemba 20, 2024 amezindua na kukabidhi nyumba 109 kwa waathirika wa maafa ya maporomoko ya tope yaliyotokea Desemba 03, 2023 Hanang, mkoani Manyara.
Nyumba hizo ambazo zimejengwa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kushirikiana na Shirika la Msalaba Mwekundu na Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) zipo katika kijiji cha Wareti, Wilaya ya Hanang mkoani Manyara.
Ujenzi wa nyumba hizo ulitokana na maamuzi ya Rais Dkt. Samia baada ya kutembelea eneo lililoathiriwa na maporomoko ya tope. Uamuzi huo ni muendelezo wa dhamira ya dhati ya Serikali ya kuwalinda wananchi wake na kurejesha hali ili waendelee na mfumo wa maisha baada ya maafa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news