ARUSHA-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Desemba 06, 2024 anafungua Kongamano la Kimataifa la 14 la Taasisi ya Wahandisi Tanzania (IET).
Kongamano hilo linalifanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) limelenga kuwakutanisha Wahandisi na Mafundi Sanifu kutoka Taasisi za Serikali na Sekta Binafsi kwa lengo la kujifunza, kujadili, kutathmini na kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya kihandisi.