DODOMA-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Desemba 12, 2024 anafungua mkutano Mkuu wa 19 wa Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania, katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma.
Mkutano huo unatoa fursa kwa wakuu wa shule kufanya tathmini ya utendaji kazi kwa mwaka mzima na kubadilishana uzoefu katika masuala mbalimbali ya usimamizi na uendeshaji wa elimu nchini. Kauli mbiu ya Mkutano huo ni _TEHAMA ni ufunguo katika kutekeleza mitaala na kutengeneza fursa za ajira Tanzania._