ARUSHA-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Desemba 20, 2024 atazindua Tuzo za Uhifadhi na Utalii katika Ukumbi wa Hoteli ya Mt. Meru Arusha.
Tuzo hizo zitasaidia kuchochea ushindani mzuri kati ya wadau wa sekta ya maliasili na utalii na hatimaye kuwezesha kuboresha utoaji huduma, kuhifadhi mazingira hivyo kuchangia katika kukuza sekta.