Waziri Mkuu mgeni rasmi ufunguzi wa Kongamano la Wafamasia
DODOMA-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Desemba 4, 2024 ni mgeni rasmi katika ufunguzi wa kongamano la Kisayansi na mkutano wa 54 wa Chama cha Wafamasia Tanzania.
Kaulimbiu ya Mkutano huo unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete, Jijini Dodoma ni "Ubunifu kwa Mustakabali wa Huduma za Afya Tanzania."