DAR-Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana,Ajira na Watu wenye Ulemavu, Mhe.Ridhiwani Kikwete leo amefanya mazungumzo na timu ya wataalam wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi nchini (WCF) kuhusu utekelezaji wa sheria ya kulipa mafao.
"Nimetumia sikukuu ya Uhuru wa Nchi yetu leo tarehe 9 Desemba 2024, kujadiliana na Timu ya wataalam wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi Nchini kuhusu utekelezaji wa sheria ya kulipa mafao na fidia kwa wafanyakazi wanapopata changamoto kazini na kupelekea madhara ya muda mfupi na yale Kudumu.
"Mabadiliko haya yanalenga kutatua changamoto zinazosababisha baadhi ya Wafanyakazi kushindwa kurudi katika hali zao za kawaida punde changamoto za ajali kazini zinapotokea."