DAR-Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,Mhe. Ridhiwani Kikwete leo Desemba 1,2024 ameongoza matembezi yanayojulikana kama Sunset Walk kuunga mkono Taasisi ya Wenye Ualbino Tanzania (TAS) na Rotary Club kuchangia fedha kusaidia kupatikana kwa mahitaji muhimu kama mafuta ya ngozi, kofia kinga na mengineyo.
Waziri katika hotuba yake amewakumbusha juhudi mbalimbali zinazofanywa na Serikali ikiwemo mpango kazi wa kupambania haki za wenye ulemavu wakiwemo wenye Ualbino utakaozinduliwa hivi karibuni.