DAR-Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Mhe. Ridhwani Kikwete leo ameshiriki kikao na wadau wa maendeleo kwa ajili ya utekelezaji wa Awamu ya Tatu ya Mradi wa Kuondoa Umaskini kilichoongozwa na Wizara ya Fedha, Benki ya Dunia na nchi marafiki wa maendeleo.