PWANI-Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,Mhe. Ridhiwani Kikwete ameshiriki Maulid ya Kumswalia Mtume Muhammad (Amani Imuendee) iliyofanyika Mkuranga, Pwani chini ya Alhaj Mheshimiwa Abdallah Ulega.

Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete ambaye pia ni Mbunge wa Chalinze amemshukuru Mwenyezi Mungu kwa fursa ya kuhudhuria na kupata nafasi ya kushiriki kaswida na Madrasa yake ya Qadiriyah ya Bagamoyo kwa Sheikh Ramiyah.