Waziri Silaa aelezea manufaa ya Chuo cha TEHAMA Dodoma

DAR-Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry Silaa, ametangaza kuwa serikali iko katika hatua za mwisho za kuanza ujenzi wa Chuo Mahiri cha Tehama (Digital Technology Institute) mjini Dodoma.
Amesema kuwa, ujenzi wa chuo hicho unatekeleza maono na maelekezo ya Rais Mhe. Dk. Samia Suluhu Hassan ya kuendeleza sekta ya TEHAMA na kuwafaidisha vijana wenye ubunifu katika fani za TEHAMA.

Kauli hii ilitolewa Desemba 5, 2024 wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi za TCRA, jijini Dodoma.

Aliongeza kuwa hatua mbalimbali zimekamilika serikalini, na Wizara hiyo imekamilisha hatua kadhaa za maandalizi ya awali ikiwa ni pamoja na kupata eneo la ujenzi wa chuo hicho lililopo Nala, mkoani Dodoma lenye hekari 400, ambalo tayari lina hati ya umiliki.
“Chuo hiki kitakuwa na lengo la kuwasaidia vijana wabunifu kutoa suluhu za kiteknolojia kwa matatizo mbalimbali katika sekta za kilimo, kifedha, na afya pamoja na kusaidia vijana kujiajiri na kuwapa maarifa ya kuanzisha kampuni na kuendeleza bunifu zao katika maeneo ya majaribio,”amesema Waziri huyo.

Sambamba na hilo amesema kazi kubwa ya chuo hiki ni kukuza vipaji katika fani za TEHAMA na kuhakikisha bidhaa za TEHAMA zinazozalishwa zinapata soko la ndani na nje ya nchi.

“Mradi huu una pande mbili, upande mmoja unatekelezwa chini ya mradi mkubwa wa Tanzania ya Kidijitali kwa ufadhili wa Benki ya Dunia, na upande wa pili kwa ushirikiano na Korea Exim Bank chini ya Serikali ya Jamhuri ya Korea ikiwa ni matokeo ya ziara za viongozi, ikiwemo Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa nchini Korea,” amezungumza Waziri Silaa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news