Waziri Suleiman afungua Mkutano wa Saba wa Umoja wa Vyama vya Siasa barani Afrika (APCA)



ZANZIBAR-Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema,kukaa pamoja viongozi wa vyama vya siasa barani Afrika watapata nafasi pana ya kuzungumza masuala mbalimbali ya vyama vyao ili kukuza suala zima la demokrasia nchini.
Akifungua kikao cha Mkutano wa Saba wa Umoja wa Vyama vya Siasa barani Afrika (APCA),Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala bora, Mwl. Haroun Ali Suleiman kwa niaba ya Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi katika ukumbi wa Hoteli ya Marijani Kiwengwa Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Amesema, katika nchi ni muhimu kuzungumza na kuyajadili masuala ya kudumisha amani, utulivu na utawala bora kwa maslahi ya wananchi na maendeleo kwa ujumla.
"Sisi Zanzibar na Tanzania kwa ujumla tumefanikiwa kuwepo utawala bora, amani na utulivu na ndio maana tumeweza kuunda Serikali ya umoja wa kitaifa,"alisema Waziri Haruon.

Hata hivyo, amesema katika mkutano huo kutajadiliwa na kuzungumzia masuala ya hali za nchi na mabadiliko ya kisiasa Afrika katika chaguzi zinazofuata pamoja na kufundishana na kusaidiana njia za utawala bora na uwajibikaji katika bara la Afrika.
Naye Mwenyekiti wa APCA Afrika kutoka nchini Kenya, Duncan Kupngeno amesema, watakuwepo hapo kujadili na kusaidiana katika masuala ya siasa ili kila nchi kutoa uzoefu wao kisiasa kwania yakupiga hatua kubwa kimaendeleo.

Hata hivyo amesema, mkutano huo utawasaidia kuona viongozi wa Afrika wanafuata demokrasia kwa utaratibu mzuri wa kuhudumia watu wanavyo waongoza.
Mkutano huo wa siku mbili wa umoja wa vyama vya siasa barani Afrika ambapo viongozi wa Nchi mbali mbali wamehudhuria ikiwemo Afrika na nchi kutoka Bara la Ulaya marekani na uengereza kujadili mfumo mzima wa vyama vyao vya siasa na kuitembelea Zanzibar katika maeneo yake ya kihstoria.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news