Wizara yafunga mwaka kwa kuzindua tuzo za kitaifa za Utalii na Uhifadhi

NA JOHN MAPEPELE

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi amesema Serikali kwa mara ya kwanza katika historia Desemba 20, mwaka huu inakwenda kuzindua tuzo za sekta ya Utalii na Uhifadhi.
Akizungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari, Dkt. Abbasi amesema,wizara imeamua kufanya hiyo ili kutoa hamasa kwa wadau wa sekta hizo waweze kufanya vizuri hivyo kuchangia kwenye uchumi wa taifa.

Amefafanua kuwa, ujumla ya tuzo 11 za heshima zitatolewa kwa wadau mbalimbali kutambua mchango wao katika sekta hizo.
Aidha, ameongeza kuwa Tanzania imeendelea kufanya vizuri katika kupokea watalii wa kimataifa na kuvunja rekodi zilizowekwa kabla ya kipindi cha UVIKO-19 mwaka 2019.

"Kwa mujibu wa Ripoti ya Nusu Mwaka ya Takwimu za Utalii ya Shirika la Utalii Duniani (UN Tourism Barometer report) katika kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Julai, 2024, Tanzania imeshika nafasi ya kwanza Afrika kwa nchi zilizotembelewa na idadi kubwa ya watalii,"amefafanua Dkt.Abbasi.
Aidha, amesema tukio la uzinduzi wa tuzo hizo utaambatana na burudani mbalimbali za wasanii.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news