Yanga SC yaichapa Fountain Gate FC mabao 5-0

DAR-Mabingwa wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara, Young Africans Sports Club (Yanga SC) imewachapa Fountain Gate FC mabao 5-0.
Kipigo ambacho kimetajwa kuwa chenye maumivu mazito kwa wana Fountain Gate ambao awali walifanyiwa maombi huko mkoani Manyara.

Yanga SC imetembeza kichapo hicho leo Desemba 29,2024 katika uwanja wa KMC Complex uliopo Mwenge katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Pengine, Gusa Achia Twende Kwao ya Kocha Mkuu wa Yanga SC, Sead Ramovic imekuja katika kipindi ambacho wengi walianza kuikatia tamaa Yanga SC.

Bao la kwanza lilifungwa dakika ya 16 na Pacôme Zouzoua, dakika ya 41 Mudathir Yahya Abbas aliweka nyavuni bao la pili.

Aidha,kabla ya kipindi cha kwanza kutamatika Pacome amerejea tena dakika ya 45' kwa kufunga bao la tatu.

Bao la nne ni la kujifunga la Jackson Katanga Shiga (OG) dakika ya 51 huku Clement Mzize akifunga hesabu dakika ya 87 kwa bao la tano.

Yanga SC ambao wapo nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi imefunga jumla ya magoli 32 huku ikiruhusu magoli sita na kukusanya alama 39 baada ya mechi 15 za mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news