Yanga SC yaichapa Namungo FC mabao 2-0, Mashujaa FC yatoka sare na Kagera Sugar bao 1-1

LINDI-Young Africans Sports Club (Yanga SC) imeichapa timu ya Namungo FC kutoka Ruangwa mkoani Lindi mabao 2-0.
Ni kupitia mtanange wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara ambao umepigwa Novemba 30,2024 katika Dimba la Majaliwa lililopo Ruangwa mkoani Lindi.

Mtanange huo ambao ulianza kwa timu zote kukamiana vilivyo, dakika 45 za kwanza zilitamatika kwa pande mbili kwenda mapumziko huku ubao ukisoma sifuri.
Kennedy Musonda dakika ya 50 ndiye aliyeanza kwa kulipa bili ya waajiri wake Yanga SC ambao katika siku chache mambo yalikuwa magumu kwao.

Dakika ya 67, Zouzoua Peodoh Pacome naye alilipa bili tena kwa waajiri wake Yanga SC kwa kupachika bao lingine ambalo lilidumu hadi dakika 90 zinatamatika.
Awali, Yanga SC ilianza kukatiwa tamaa baada ya kupoteza mechi tatu mbili ziliwa ni za Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara na moja ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika.

Kichapo cha kwanza kilitoka kwa Azam FC ambapo mtanange huo uliisha kwa bao 1-0 huku warina asali wa Tabora, Tabora United FC ikiwachapa mabao 3-1 katika mtanange huo wa ligi kuu.
Aidha, katika mtanange wa Ligi ya Mabingwa barani Afrika waliambulia kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Al Hilal Omdurman ya Sudan.

Kwa matokeo ya Novemba 30,2024 Yanga inatinga katika nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara ikiwa na alama 27 huku watani zao Simba SC ikiwa kileleni kwa alama 28.
Wakati huo huo, Mashujaa FC imegawana alama moja na Kagera Sugar FC baada ya matokeo ya bao 1-1 katika mtanange wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara.

Mtanange huo umepigwa Novemba 30,2024 katika Dimba la Tanganyika lililopo mkoani Kigoma ambapo bao la Mashujaa FC lilifungwa na Mohamed Saleh Mussa kwa penalti dakika ya 88.

Aidha, Kagera Sugar bao lao lilifungwa dakika ya 31 na Tariq Seif Kiakala

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news