ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi amelihakikishia Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) kuwa, Zanzibar ipo tayari na inajiandaa vema kufanikisha Mashindano ya CHAN yanayotarajiwa kufanyika Februari,mwakani.


Rais Dkt.Mwinyi amesisitiza kuwa, mbali na viwanja pia Serikali inajiandaa na kuwa na hoteli bora na za kutosha zitakazokuwa na uwezo wa kupokea wageni watakaofika kwa ajili ya mashindano hayo na huduma bora.

Pia,Rais Motsepe amesifu juhudi zinazoendelea za kuimarisha viwanja vya ndege, miundombinu ya barabara na ongezeko la hoteli mambo aliyosema kuwa ni muhimu katika kufanikisha mashindano.