Zanzibar kuwa kivutio kikubwa cha Utalii wa kisasa-Rais Dkt.Mwinyi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inakusudia kuifanya Zanzibar kuwa kituo kikubwa cha Utalii wa kisasa usio na misimu kwa kuwavutia wawekezaji na wageni wengi.Rais Dkt.Mwinyi ameyasema hayo Ikulu Zanzibar alipozungumza na Balozi mpya wa Uingereza nchini Tanzania Mhe. Marianne Young aliyefika kujitambulisha.

Aidha,Rais Dkt.Mwinyi amesema bado ina Zanzibar ina mahitaji makubwa ya uwekezaji kwenye sekta ya Uchumi wa Buluu kupitia Utalii, Bandari, Mafuta na gesi pamoja na sekta ya usafirishaji wa majini.
Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi amesema dhamira ya Serikali ni kuwa na Utalii wa hadhi ya juu utakaowavutia wageni wengi kuja nchini bila kujali misimu ya utalii, pia amesema nchi imejiandaa kuwa na misimu yote ya Utalii kwa kuimarisha vivutio zaidi vyenye kuwavutia wageni wengi.

Hata hivyo, Rais Dkt.Mwinyi amewakaribisha wawekezaji zaidi wa Uingereza kuja Zanzibar kwa wingi kuwekeza na kunufaika na fursa za uwekezaji zilizopo.
Pia amewaalika wawekazaji wa sekta binafsi wa Uingereza kuitembelea Zanzibar kubaini uzuri na fursa zilizopo.

Wakati huo huo, Rais Dkt. Mwinyi ameishukuru Serikali ya Uingereza kwa ushirikiano wa diplomasia uliopo baina yao na Tanzania ikiwemo Zanzibar pia kwa kuisaidia Zanzibar kwa sekta mbalimbali ikiwemo Elimu, Afya na masuala mengine ya jamii.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news