ZANZIBAR-Zoezi la utambuzi wa Vipaji kwa Vijana waliozaliwa Mwaka 2010 hadi 2013 limefanyika katika Mkoa wa Kaskazini Unguja, Kwenye Uwanja wa Cairo.
Zoezi hilo limeeendelea vyema chini ya usimamizi wa ujumbe kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu la Dunia (FIFA). Kwa upande wa Pemba, zoezi hilo litafanyika kuanzia Desemba 8 hadi 9,2024 kwa Mkoa wa Kusini Pemba.Zoezi hilo litahitimishwa Kaskazini Pemba, Desemba 10 hadi Desemba 11,2024.