Afisa Misitu apandishwa kizimbani kwa tuhuma za rushwa

MANYARA-Januari 14, 2025 Afisa Misitu wa Jumuiya ya uhifadhi msitu wa SULEDO, Bw. Siloma Manyindo Mtero amefikishwa mahakamani na kufunguliwa shauri la jinai namba 03/2025.
Ni kwa makosa ya kuomba na kupokea Rushwa kinyume na kifungu cha 15(1)(a) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa sura ya 329 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2022.

Sambamba na kosa la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kinyume na kifungu cha 302 cha Kanuni ya Adhabu, sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2022.

Mshtakiwa huyo aliomba rushwa kiasi cha shilingi 600,000 kutoka kwa Mwenyekiti wa Kitongoji cha Ndilali ili awaruhusu baadhi ya wananchi wa kitongoji hicho kufanya shughuli za kilimo ndani ya msitu wa SULEDO.

Shauri tajwa limesomwa mahakamani na Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU, Wakili Yahaya Masakilija mbele ya Hakimu Mkazi wa Wilaya ya Kiteto,Mheshimiwa Aron Losioki.

Mshtakiwa amesomewa hati ya mashtaka na amekana mashtaka yote yanayomkabili, lakini amepelekwa mahabusu baada ya kushindwa kukidhi masharti ya dhamana.

Shauri hili limepangwa tena Januari 28,2025 kwa ajili ya kusikilizwa hoja za awali (PH).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news