Ajali ya lori yaua 11 Handeni

TANGA-Watu 11 wamefariki dunia wa Kijiji cha Chang’ombe kilichopo Kata ya Segera wilayani Handeni mkoani Tanga baada ya kugongwa na lori lililokuwa limebeba saruji.

Ni baada ya kupoteza uelekeo wakati walipojitokeza barabarani walipokuwa wakishanga ajali ya gari dogo aina ya Tata.

Watu hao walijitokeza barabarani ili kuweza kutoa msaada kufuatia ajali ya barabarani ya gari dogo aina ya Tata ndipo walipokumbana na ajali hiyo iliyopelekea kupoteza maisha.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Batilda Burian lori hilo liliwagonga watu hao usiku wa kuamkia Januari 14,2025 na kusababisha vifo hivyo pamoja na majeruhi.

Lori hilo lenye namba za usajili T.680 BQW likiwa linatokea Tanga lilifeli breki na kuwagonga watu waliokuwepo pembezoni mwa barabara na kusababisha vifo vya watu 11 papo hapo na kujeruhi wengine 11.

Miili ya marehemu hao imehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Korogwe Magunga na majeruhi wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news