Akiba Commercial Bank Plc yawazawadia washindi wa Kampeni ya Twende Kidijitali Tukuvushe Januari

DAR-Akiba Commercial Bank (ACB) Plc imewashukuru wateja wake kwa kushiriki katika Kampeni ya Twende Kidijitali Tukuvushe Januari.Pia, imewahimiza kuendelea kutumia huduma zake za kidijitali kama vile ACB Mobile, Internet Banking, ACB VISA Card, na ACB Wakala ili kufurahia uzoefu wa kipekee wa kibenki.

Shukrani hizo zimetolewa jijini Dar es Salaam Januari 16,2025 na Mkuu wa Kitengo cha Biashara cha Akiba Commercial Bank Plc,Dkt. Danford Muyango wakati wa hafla ya kuwazawadia washindi wa Kampeni ya droo ya kwanza ya kampeni ya Twende Kidijitali, Tukuvushe Januari.

Wateja kadhaa kutoka Dar es Salaam na mikoani walipokea zawadi za fedha zilizowekwa moja kwa moja kwenye akaunti zao pamoja na zawadi nyinginezo.
"Kampeni ya Twende Kidijitali, Tukuvushe Januari ilizinduliwa katikati ya Desemba 2024 kwa lengo la kuboresha mazingira ya kibenki kwa wateja wakati wa msimu wa sikukuu na pia kuwasaidia wateja kushinda changamoto za kifedha mwezi huu kupitia zawadi mbalimbali, hivyo droo hii haitaishia hapa ni endelevu,"amesema Danford.

Wateja walionesha furaha na shukrani kwa Akiba Commercial Bank kwa jitihada zake za kuimarisha huduma za kidijitali ambazo zimeboresha uzoefu wao wa kibenki,kwa kuwapatia urahisi na wepesi wa kupata huduma za kifedha wakiwa mahali popote na wakati wowote.

Miongoni mwa wateja akizungumza katika hafla ya kukabidhiwa zawadi hizo, Bw. Alfayo Zephania alieleza jinsi alivyopokea kwa furaha habari njema za kuibuka mshindi wa kampeni hiyo.

"Nilifurahishwa sana na taarifa ya ushindi wangu na ninaishukuru Benki ya Akiba kwa kujali wateja wake na kutoa huduma bora na ninatoa rai kwa watu wengine kujiunga na Akiba Commercial Bank wanufaike na mengi ikiwemo mikopo ambayo imenivusha pakubwa katika biashara zangu.”

Naye mteja Ezekiel Willium alielezea furaha yake kwa zawadi aliyoshinda, akisema kuwa ushindi huo umempa hamasa zaidi ya kushiriki kwa bidii ili kupata zawadi kubwa zaidi katika droo kuu ya mwisho wa kampeni.

Aidha Akiba Commercial Bank imewashukuru wateja wake kwa kushiriki katika kampeni hiyo na inawasihi waendelee kutumia huduma za kidijitali za benki .

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news