DAR-Aaliyekuwa Mhasibu wa Klabu ya Mpira wa Miguu ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni (KMC FC),Bw. Atulinda Barongo hivi karibuni alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kivukoni iliyopo Kinondoni Dar es Salaam na kufunguliwa shauri la uhujumu uchumi Namba 1099/2025.
Katika shauri hili Bw. Barongo anashtakiwa kwa kufanya ubadhirifu wa fedha kiasi cha Tshs. 12,000,000/= kinyume na kifungu cha 28(1) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329 kama ilivyorejewa mwaka 2022.
Pia ameshtakiwa kwa kosa la kutumia nyaraka kumdanganya mwajiri wake kinyume na kifungu cha 22 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na rushwa Sura ya 329 Rejeo la 2022.
Mshtakiwa huyo alisomewa mashtaka na Mwendesha Mashitaka wa TAKUKURU Wakili Janeth Kafuko na shauri hili linasikilizwa na Mh. Hakimu Nabwike Mbarouk.
Shauri limepangwa kuanza kusikilizwa hoja za awali (PH) tarehe 3/2/2025.
Tags
Habari
Kinondoni Manispaa
KMC FC
Mahakamani Leo
Michezo
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)