Aliyeshiriki kusambaza picha za utupu kuhusu Shule ya Sekondari Baobab akamatwa

PWANI-Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linamshikilia mtu mmoja anayetuhumiwa kusambaza picha za mjongeo zenye maudhui machafu.

Ni picha ambazo zimeunganishwa na majengo ya Shule ya Sekondari ya Baobab, hali iliyosababisha taharuki miongoni mwa wazazi na wafanyakazi wa shule hiyo iliyopo mkoani Pwani.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Pwani, Salim Morcase amesema, picha hizo zilisambazwa kuanzia Desemba 31, 2024 na zilionesha wasichana wakiwa na nywele za bandia.

Ikiwa ni tofauti na wanafunzi wa shule hiyo ambao hufuata utaratibu wa kusuka nywele za asili kwa mtindo wa twende kilioni.

Kamanda Morcase ameeleza kuwa,mtuhumiwa huyo anashikiliwa kwa tuhuma za kutengeneza na kusambaza picha hizo kwa nia ya kuaminisha umma kuwa vitendo hivyo vinafanywa na wanafunzi wa shule hiyo.

“Jeshi la Polisi lilipokea taarifa rasmi kutoka kwa uongozi wa shule ya Baobab mnamo Januari 3, 2025, na tumeanza kuchukua hatua za kuwafuatilia na kuwasaka watu wengine waliohusika,” amesema Kamanda Morcase.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Shajar, inayomiliki shule hiyo, Shani Swai, amesema picha hizo ziliibua hofu kubwa kwa wazazi na wafanyakazi wa shule.

"Kutokana na ukosefu wa utaalamu wa kuchunguza picha hizo, tuliamua kuwasilisha suala hili kwa Jeshi la Polisi ili wachukue hatua stahiki," amesema Swai.

Mwenyekiti wa Bodi ya Taaluma ya shule hiyo, Mhandisi Fredy Ntevi, amebainisha kuwa picha hizo zilionyesha wasichana wakiwa wamesuka nywele za bandia, jambo ambalo halilingani na utaratibu wa shule hiyo, ambapo wanafunzi wote hufuata mtindo wa nywele wa asili.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news