ATCL yatangaza nafasi 50 za ajira

DAR-Shirika la Ndege la Air Tanzania Company Limited (ATCL) limetangaza nafasi zaidi ya 50 za ajira kama sehemu ya mkakati wake wa upanuzi, likitoa fursa kwa Watanzania wenye sifa kujiunga na shirika hili.

Nafasi hizi zinapatikana katika idara mbalimbali, zikiwemo Uendeshaji wa Ndege, Upangaji wa Ratiba za Wahudumu wa Ndege, Mauzo na Masoko, Usaidizi wa Rampu, na Udereva.
Afisa Uendeshaji wa Ndege Daraja la II (Nafasi 5) – Mwombaji anapaswa kuwa na leseni ya TCAA au ICAO ya Flight Dispatcher. Afisa Upangaji wa Ratiba za Wahudumu wa Ndege Daraja la II (Nafasi 2) – Nafasi inapatikana kwa wenye Shahada pamoja na cheti cha masuala ya usafiri wa anga.

Madereva (Nafasi 37) mwombaji anatakiwa kuwa na Cheti cha Kidato cha Nne na leseni halali ya daraja C1 au E pamoja na uzoefu wa angalau mwaka mmoja.

Afisa Mauzo na Masoko II (Nafasi 2) – Mwombaji anapaswa kuwa na Shahada pamoja na cheti cha masuala ya anga, kama vile Air Transport Management.

Msaidizi wa Rampu Daraja la II (Nafasi 12) – Mwombaji anapaswa kuwa na Cheti cha Elimu ya Sekondari na cheti cha masuala ya anga.

Zoezi la ajira linakusudia kusaidia upanuzi wa ATCL kwa kuboresha utoaji wa huduma na ufanisi wa shirika. Waombaji wenye sifa wanapaswa kutuma maombi kupitia Tovuti ya Ajira ya ATCL ndani ya siku 14 tangu kutangazwa kwa nafasi hizi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news