Balozi Kasike afanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa ATCL

DAR-Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji,Mhe.Phaustine Kasike amekutana na Mkurugenzi Mkuu wa ATCL, Mhandisi Peter Ulanga.
Mkutano huo umefanyika Januari 30,2025 kwenye Ofisi za ATCL zilizopo eneo la Uwanja wa Ndege wa Zamani Dar es Salaam (Terminal One).

Katika mazungumzo yao, Mhandisi Ulanga ameeleza nia ya Shirika la ATCL kuanza safari za kwenda nchini Msumbiji ili kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kijamii baina ya nchi hizo mbili zenye uhusiano wa kidugu na kihistoria.
Aidha, Mhandisi Ulanga ameongeza kuwa ATCL inadhamiria kuanzisha mchakato hivi karibuni wa kushughulikia taratibu za kitaalamu zinazohitajika kuwezesha safari hizo kuanza.

Kwa upande wake, Mhe. Balozi Kasike aliahidi kutoa kila aina ya ushirikiano kwa ATCL ili kufanikisha azma hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news