BONDIA wa ngumi za kulipwa kutoka Tanzania, Emmanuel Mwakyembe ampoteza pambano lake dhidi ya mpinzani wake Tigran Uzlyan wa Urusi.
Mwakyembe amepoteza pambano hilo lililofanyika nchini Urusi la raundi 10 kwa 'points' dhidi ya bondia Uzlyan raia wa nchi hiyo.
Mwakyembe ni bondia mwenye hadhi ya nyota mbili akiwa na rekodi ya kucheza mapambano 15 akishinda 12 matatu kwa 'KO', kupoteza mawili na kutoka sare mawili.
Pia Mwakyembe ni bondia namba 152 kati ya mabondia 2,503 Duniani huku nchini Tanzania akiwa namba nne kati ya 115 katika uzito wa light.
Kabla ya kupoteza pambano hilo la Januari 22 mwaka huu mara ya mwisho Mwakyembe kupoteza pambano ilikua ni Agosti 14, 2020 alipopigwa na Juma Choki kwa 'points' za majaji wote watatu kwenye pambano lililofanyika katika ukumbi wa Mlimani City.
Na kwa upande wake Uzlyan ni bondia mwenye hadhi ya nyota tatu akiwa amecheza mapambano 11 akishinda 10 na sita kati ya hayo kwa 'KO' na kupoteza moja kwa 'points' huku akiwa bondia namba 50 kati ya mabondia 2,503 Duniani na nchini kwao Urusi ni wa tatu kati ya mabondia 33.